Kipaza sauti wakati wa matabano

Swali: Kuna baadhi ya wasomaji huwafanyia watu matabano na hutumia kipaza sauti. Je, kitendo hichi ni katika Bid´ah au ada za kawaida?

Jibu: Matabano yaliyowekwa katika Shari´ah ni kumsomea mgonjwa moja kwa moja na kumpulizia cheche za mate pasi na simu wala kipaza sauti. Lakini baadhi ya watu wanachotaka ni kujizidishia kutokana na ile bonasi ya pesa wanayopata kutoka kwa wale wagonjwa. Matokeo yake ndio hutumia mfano wa vifaa hivi kwa ajili ya wingi wa wateja. Lengo lao ni pesa tu. Watu sampuli hii matabano yao kuwafanyia wagonjwa hakunufaishi kitu. Kwa sababu inatumiwa njia ambayo haikuwekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 49
  • Imechapishwa: 06/06/2021