Swali: Baada ya kufungua swalah na baada ya kuzama kwa jua, akaenda mwanamke ili kutawadha kwa ajili ya kuswali ambapo akaona kuwa amepata ada yake ya mwezi. Je, funga yake ni sahihi?

Jibu: Kama amepata damu baada ya jua kuzama, basi funga yake ni sahihi. Ikiwa hakujua kuwepo kwa damu isipokuwa baada ya jua kuzama, basi funga yake ya siku hiyo ni sahihi. Lakini kama ni mwenye uhakika kuwa damu ilimjia kabla ya jua kuzama, basi funga yake haisihi. Katika hali hiyo atalazimika kuilipa. Hili ni lazima litambulike.

Kwa hiyo ikiwa damu ilimjia baada ya kuzama kwa jua, swawm yake ni sahihi. Na kama hakulijua hilo isipokuwa baada ya kuzama kwa jua, basi funga yake ni sahihi. Lakini akijua kama damu ilimjia kabla ya jua kuzama, basi atalazimika kuilipa siku hiyo.

Swali: Katika hali hii mwanamke hakujua isipokuwa wakati alipoenda kutawadha baada ya kufungua swawm. Kwa hiyo halazimiki kuilipa funga hiyo?

Jibu: Swawm yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/5427/حكم-من-جاءتها-الدورة-بعد-الغروب-في-رمضان
  • Imechapishwa: 06/06/2021