Khatari ya kuamrisha mema lakini mtu hayafanyi

Swali: Hadiyth iliyo kabla yake inayozungumzia ambao watakuwa Motoni:

” Ataletwa mtu siku ya Qiyaamah na kuvugumizwa Motoni … ”?

Jibu: Hiyo ni Hadiyth ya Usaamah ya kwamba:

“Ataletwa mtu siku ya Qiyaamah na kuvugumizwa Motoni ambapo matumbo yake yatatoka nje. Atazunguka nayo kama punda anavozunguka kwenye kinu chake. Watu wa Motoni watakusanyika kwake na kusema: “Ee fulani! Una nini? Wewe si ulikuwa ukiamrisha mema na ukikataza maovu?” Aseme: “Nilikuwa nikikuamrisheni mema lakini mimi mwenyewe siyafanyi na nikikukatazeni maovu lakini lakini mimi mwenyewe nayafanya.”[1]

Anawaambia watu waswali lakini yeye haswali, anawakataza watu kuzini lakini yeye anazini na anawakataza watu kunywa pombe lakini yeye anakunywa pombe. Tunamuomba Allaah afya.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (124).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21538/جزاء-من-يامر-بالمعروف-ولا-ياتيه
  • Imechapishwa: 20/08/2022