Deni la kafiri baada ya kusilimu

Swali: Je, deni la kafiri linabaki anaposilimu?

Jibu: Madeni ya watu yanabaki. Anatakiwa kuwarudishia ikiwa anawajua. Uislamu haudondoshi deni. Anatakiwa kuwapa watu haki zao. Uislamu unadondosha haki ya Allaah. Allaah anasamehe yale maovu yote yaliyotangulia. Lakini ikiwa yuko na mali, amana na haki za watu basi anatakiwa kuzirudisha.

Swali: Vipi ikiwa wako mbali?

Jibu: Azitume kwa njia ambayo anataraji zitawafikia.

Swali: Ikiwa ni makafiri ambao kuna vita kati yetu sisi na wao ambapo alichukua deni kwao kabla ya kusilimu?

Jibu: Haijalishi kitu. Udhahiri ni kwamba anatakiwa kuwapa haki zao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21563/هل-يسقط-الدين-على-الكافر-اذا-اسلم
  • Imechapishwa: 20/08/2022