Kama al-Albaaniy angelikuwa ni Murjiy basi Maalik, ash-Shaafi´iy na Ahmad nao wangelikuwa ni Murji-ah

Swali: Mwenye kusema kuwa asiyeswali hakufuru ameyaondosha matendo nje ya imani na hivyo maoni yake yameafikiana na ya Murji-ah?

Jibu: Hapana. Si kweli. Wako wanachuoni wengi wenye kuona kuwa mwenye kuacha swalah hakufuru. Miongoni mwao wako wenye kusema kuwa matendo ni sehemu katika imani. Yule mwenye maoni hayo hazingatiwi kuwa ni katika Murji-ah. Hawamkufurishi kwa sababu wamezifahamu dalili kwa njia yao. Kwa hivyo si kweli kwamba kila ambaye hamkufurishi mwenye kuacha swalah ni Murji-ah. Kwani wanachuoni wengi wanaonelea hivo. Kutokana na hayo ndio kumejengeka tuhuma zilizoko hii leo zinazomtia Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika Irjaa´ kwa sababu haonelei kuwa ni kafiri. Hili ni kosa. Mambo yangelikuwa hivo basi wanachuoni wote waliotangulia wa kale ambao hawamkufurishi ambaye haswali wangelikuwa ni Murji-ah, jambo ambalo haliwezekani.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=143722
  • Imechapishwa: 01/12/2020