Je, inafaa kukata miti yenye kuudhi makaburini?

Swali 125: Je, inafaa kukata miti yenye kuudhi makaburini?

Jibu: Inatakiwa kukatwa. Inawaudhi wenye kuja kutembea. Vivyo hivyo inatakiwa kuondoa ile miiba inayopatikana kwa ajili ya kuwapumzisha watembezi kutokamana na shari yake. Haikusuniwa kwa yeyote kupanda katika makaburi chochote katika mti wala majani. Allaah hakuweka Shari´ah ya jambo hilo.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka miti miwili juu ya makaburi mawili aliyojua kuwa yanaadhibiwa. Hakupanda miti hiyo katika makaburi mengine ya Madiynah na makaburi ya al-Baqiy´. Vivyo hivyo Maswahabah hawakufanya hivo. Hivyo ikatambulika kuwa jambo hilo ni maalum kwa watu wawili wale waliokuwa wakiadhibiwa ndani ya makaburi yale.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (13/361)
  • Imechapishwa: 11/11/2021