Swalah ya Sunnah ni Rak´ah mbilimbili na sio nne

Swali: Nilisema “Allaahu Akbar” kwa ajili ya kutekeleza Sunnah kabla ya swalah ya Dhuhr na nikanuia kuiswali Rak´ah nne kwa Tasliym moja. Baada ya kumaliza kuswali Rak´ah moja kukakimiwa swalah. Je, nibadilishe nia na niswali Rak´ah mbili au niikate?

Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Kunapokimiwa swalah basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile ya faradhi.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Kwa hiyo kilichowekwa katika Shari´ah pindi kunapokimiwa swalah na wewe waswali swalah iliyopendekezwa, basi uikate kutokana na Hadiyth hii tukufu.

Pia imesuniwa kwa muislamu kuswali swalah zilizopendekezwa Rak´ah mbilimbili; mchana na usiku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Imekuja katika upokezi ambao ni Swahiyh:

“Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa as-Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Lakini endapo swalah itakimiwa na yeye yuko katika Rukuu´ ya mwisho ya Sunnah au katika Sujuud ya mwisho bora ni kuikamilisha. Kwa sababu hakukubaki isipokuwa kitu kidogo kilicho chini ya Rak´ah. Uchache wa swalah ni Rak´ah moja.

[1] Ahmad (9563), Muslim (710) na Abu Daawuud (1266).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/389)
  • Imechapishwa: 11/11/2021