Imamu kuwaeleza maamuma kuwa yeye ni msafiri

Swali: Ni lini imamu anatakiwa kusema:

“Kamilisheni swalah zenu. Kwani hakika mimi ni msafiri.”?

Jibu: Ni Sunnah ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) na ni sahihi. Imamu ataisema kwa sauti ya juu baada ya yeye kutoa salamu ya kwanza kimyakimya. Miongoni mwa Sunnah ni kuacha Sunnah. Tasliym ya pili imependekezwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 175
  • Imechapishwa: 03/07/2022