Swali: Kuna mlinganizi mmoja anawapaka mchanga wa machoni ´Awwaam na khaswa vijana. Anasema kuwa ni jambo liko kwa mapendekezo ya Muislamu kuwa na ndevu kiasi akitakacho midhali hazinyoi. Fatwa yake imekuwa ni mtihani mkubwa na imewaathiri vijana wengi. Kuna wengi wanaoeneza fatwa yake ya kusikika. Ni ipi Radd ya fatwa hii?

Jibu: Fatwa hii ni mbovu na imejengwa juu ya matamanio. Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo ni Swahiyh na za wazi zinaamrisha kuacha ndevu:

“Acheni ndevu.”

“Zikirimuni ndevu.”

“Refusheni ndevu.”

“Fugeni ndevu.”

Hadiyth zote hizi ni Swahiyh na zimepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim.

Kuhusiana na Hadiyth juu ya kufupisha ndevu kwa urefu na upana, haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imekosolewa na wanachuoni. Haikuthibiti. Hivyo haitumiwi kama dalili kwa kuwepo Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Mtu huyu ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah na abainishiwe haki na asiwadanganye watu na fatwa hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015