Ibn ´Uthaymiyn mwanamke kumsahihisha mwanaume ndani ya swalah


Swali: Lau mwanamke ataswali nyuma ya wanaume kisha akakosea imamu, akakosea katika kusoma kwake Qur-aan na asisahihishwe. Lakini mwanamke akawa anajua hilo. Je, anaweza akamsahihisha?

Jibu: Ikiwa hili ni katika al-Faatihah, ni lazima kwake mwanamke kumsahihisha. Kwa kuwa lau imamu atakosea al-Faatihah swalah haitosihi. Ikiwa sio al-Faatihah na wanaume wakawa hawajui na wala hawatoshangazwa akiongea mbele yao, amrekebishe na hakuna neno. Kwa kuwa sauti ya mwanamke sio ´Awrah. Dalili kuonesha kuwa sio ´Awrah ni maneno Yake (Ta´ala):

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

“Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake; mkiwa na taqwa, basi msilainishe kauli asije akaingiwa na tamaa yule ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika.” (33:32)

Makatazo ya kutolainisha sauti ni dalili inayoonesha kuwa inajuzu kuongea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (13 A)
  • Imechapishwa: 14/09/2020