Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanamke kufanya darsa na mihadhara kwenye misikiti akiwatolea wanawake kwa njia ambayo sauti yake haitoki nje kwa wanaume?

Jibu: Hili halijulikani ya kwamba wanawake kusomesha misikitini au kutoa Khutbah kwenye misikiti. Hili halijulikani. Hichi ni kitu kipya. Wanawake wanatakiwa kujisitiri na kujiweka mbali na wanaume na wala asitoke kwenye msikitini isipokuwa kwa ajili ya kuswali. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msiwakataze wajakazi wa Allaah kwenda misikiti na majumba yao ni kheri kwao.”

Hakuna neno wakafanya mawaidha, mihadhara yenye faida wakiwa ni wenye kujisitiri au nyumbani kwake wakawa na sehemu yao maalum pasina fitina, ama kuja misikitini na kufanya darsa hili ni jambo jipya hatulijui.