Hizi sio haki za mwanamke


Haki ambazo wanadai na kwa hakika sio zake, kwa mfano uhuru wa kuvua Hijaab, kusafiri bila ya kuwa na Mahram, kuwa faragha na mwanaume, kuchanganyika na wanaume n.k., hii sio haki ya mwanamke. Haya sio mema kwa mwanamke na sio katika haki zake. Hii ni kampeni ya maadui. Wanachotaka ni kumharibu mwanamke katika jamii ya Kiislamu na wampe uhuru ambao wanadai. Uhuru unapatikana katika Shari´ah. Uhuru unapatikana katika Shari´ah. Kuvua Hijaab, kuchanganyika na wanaume, kuendesha gari, kusafiri bila ya Mahram ili aweze kuwa faragha na mwanaume, kuongea na wanaume na kuwagusa, hii sio haki yake. Mwanamke wa Kiislamu Allaah kamuweka mbali na haya. Allaah kampa haki zinazolingana na yeye Kishari´ah. Hii ndio tofauti kati ya haki za Kishari´ah na haki ambazo sio zake. Wao [maadui wa Uislamu] hawamuombei haki zake za Kishari´ah, lau wangelimuombea haki zake za Kishari´ah, kwa hakika sote tungelikuwa pamoja nao. Lakini wao wanamuombea haki za batili ambazo zinamtoa… na si haki zake, bali ziko dhidi yake na ni zenye kumletea madhara na kwa jamii.