Ibn ´Uthaymiyn kuhusu vitabu vya dini vilivyo na picha II

Swali: Ni ipi hukumu ya kuhifadhi vitabu vilivyowekwa picha mtu, ya mnyama au ya ndege? Je, tuharibu ile picha yote, kichwa peke yake au tuweke msitari shingoni tu tufanye nini pamoja na kuzingatia kwamba vitabu hivi ni vyenye faida na sio katika vitabu vya kipumbavu? Hali kadhalika magazeti ya Kiislamu.

Jibu: Picha hizi ilizoashiria kwenye vitabu na baadhi ya magazeti ya kidini, mtu akiweza kuharibu kichwa na uso wake ni jambo jema. Kwa sababu picha ni kichwa. Uhakika wa mtu unatambulika kwa kichwa chake. Mtu kama mtu anajulikana kwa kichwa na uso wake. Kutokana na hili ni lazima kuharibu kichwa na uso. Hapa ni pale ambapo mtu ataweza kufanya hivo. Ama jambo hilo likiwa gumu kwake, basi hakuna neno kwake – Allaah akitaka – na khaswa ukizingatia kwamba picha hizi mara nyingi huwa kwenye jarida la nyuma la kitabu na si kwamba inaenea na kuwa waziwazi. Kwa ajili hiyo tunaona kuwa hakuna neno ikiwak una uzito wa kuiharibu na kuiondosha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (12) https://binothaimeen.net/content/6763
  • Imechapishwa: 08/01/2021