Maskhara kwamba wamefikia kiwango cha yakini

Swali: Baadhi ya vijana wakati fulani punde kidogo kabla ya kuswali huwafanyia istihzai Suufiyyah na kusema kwamba wao wamefikia kiwango cha yakini au kwamba ´ibaadah si zenye kuwawajibikia. Je, inafaa kufanya mzaha kwa mambo kama haya hata kama kweli hufanya mambo hayo?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Analazimika kumhimidi Allaah na kumwomba amsalimishe. Asisemi maneno haya. Ni maneno ya kikafiri. Baadhi ya Suufiyyah husema kwamba ´ibaadah si zenye kuwawajibikia pindi wanapofikia katika hali hii. Muislamu ametunukiwa na Allaah neema ya Uislamu. Anawezaje basi kujiandaa na Allaah kisha akaongea maneno kama haya? Lakini endapo atanukuu maneno yao namna wanavosema, kubainisha kuwa ni batili na akazindua juu ya jambo hilo, basi hicho ni kitendo kizuri. Ama kufanya hivo punde tu kabla ya kuswali na akafanya maskhara, hakuna mambo ya maskhara katika jambo la swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 09/01/2021