Ibn Baaz kuchinja wakati wa kuhamia nyumba mpya

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchinja wakati wa kuhamia ndani ya nyumba mpya?

Jibu: Haya yalikuwa yakifanywa. Ni shirki kibwa kwa kuwa ni kuwaabudu majini.

Swali: Vipi ikiwa malengo sio kujikurubisha kwa majini?

Jibu: Ni jambo linalojulikana kuwa wanawalenga majini na wanasema kuwa wanawachinjia ili wawasalimishe na shari yao na ili wasiwaudhi katika majumba yao. Haya yalikuwa yakipatikana kusini. Lakini yameisha – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 50
  • Imechapishwa: 21/11/2016