Hii ndio sababu watu na majini wameshindwa kuleta kitu kama Qur-aan

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

“Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie maneno ya Allaah.” (09:06)

Hakusema:

“… basi mlinde mpaka asikie hikaya ya maneno ya Allaah.”

Qur-aah hii ingelikuwa ni hikaya ya maneno ya Allaah, basi Angelisema:

“… basi mlinde mpaka asikie hikaya ya maneno ya Allaah.”

Lakini badala yake Amesema:

حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

“… mpaka asikie maneno ya Allaah.”

Muumini akisikia andiko hili, basi imani yake inazidi juu ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah. Allaah (´Azza wa Jall) amezungumza kwayo kwa Ujuzi na Utashi Wake. Je, Allaah Hawezi kuzungumza? Je, maneno ni upungufu mpaka tuseme kuwa Qur-aan sio maneno ya Allaah. Kwa nini Qur-aan hii imekuwa ni miujiza na majini na watu wameshindwa kuleta mfano wake, Suurah kumi mfano wake, bali wameshindwa hata kuleta Suurah fupi mfano wake? Baada ya yote haya vipi iwe ni hikaya ya maneno ya Allaah? Haiwi kushindwa kwao isipokuwa ni kwa sababu ni maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Amezungumza kwayo kwa njia inayolingana na Yeye na kwa njia ambayo haifanani na maneno ya viumbe. Dalili juu ya hilo ni kwa kuwa majini na watu wameshindwa kuleta mfano wake, Suurah kumi au Suurah moja kama Qur-aan.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/421-422)
  • Imechapishwa: 26/08/2020