Ninamjua mtu kutoka wakati wa al-Madiynah. Kama alisikia kunaongelewa kuhusu kitabu ar-Riyaadh au Hijaaz akaenda kukinunua. Kisha akaanza kufanya kazi kama mwalimu kwenye chuo kikuu Iymaan [Swan´aa´; Yemen].

Chuo kikuu hichi ni kama vyuo vikuu vingine vyote vinavyoongozwa na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Je, wanaweza kuleta mwanafunzi mmoja aliyekhitimu ambaye amekuwa ni marejeleo? Hawawezi hilo. Hata mtu mmoja. Kila mwaka wanapokea mamilioni kama alama pekee ya taasisi hizi. Niliwauliza kuhusu tamasha (tamthili/filamu). Pamoja na hivyo wanasema ya kwamba wako katika Ahl-us-Sunnah. Nyinyi sio Ahl-us-Sunnah. Msiwadanganye watu. Wanachuoni wanasema kuwa tamasha ni haramu. Je, mmekwishaacha tamasha ambayo uharamu wake wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wamekubaliana juu yake?

al-Qaradhwaawiy – Allaah amkate ulimi wake – anashaji´isha wanawake katika tamasha[1]. Alipoambiwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy ya kwamba al-Qaradhwaawiy anasema: “Hatupigani vita na mayahudi kwa sababu ya ´Aqiydah. Tunapigana nao vita kwa sababu ya ardhi[2] [Palestina] akasema:

“Nijuacho tu ni kwamba ni Mujaahid.”

Mujaahid? Ndio, anapigana vita dhidi ya Ahl-us-Sunnah na kukimbiza watu na Sunnah na Ahl-us-Sunnah. Analingania katika upotevu. Tunaweza kusema pia kuwa ni Imaam, kiongozi. Lakini ni kiongozi mpotevu:

 وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ

“Tukawafanya viongozi wanaoita kuelekea Motoni; na siku ya Qiyaamah hawatonusuriwa.” (28:41)

Vivyo hivyo Swalaah as-Saawiy mrithi wa Sa´iyd Hawaa. Kwa masikitiko makubwa Swalaah as-Saawiy! Ninakujua tokea Misri ukiwa mtu mnyenyekevu unayeshikamana na Sunnah. Hata hivyo, umepewa mtihani kwa pesa za Saudi Arabia ukawa mmoja katika walinganiaji wa al-Ikhwaan al-Muslimuun.

[1] al-Qaradhwaawiy kasema:

“Kuna dharurah kwa mwanamke kushiriki katika tamasha”. Gazeti la Kuwaiti al-Mujtamaa

[2] Gazeti ar-Raayah (4696). Tarehe: 1415/Sha´abaan/24

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Burkaan, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 26/08/2020