Wanaopinga upokezi wa mtu mmoja katika mambo ya ´Aqiydah

Kwa kuwa kuko ambao wanasema kwamba Akhbaar-ul-Ahaad, upokezi wa mtu mmoja hautendewi kazi katika mambo ya ´Aqiydah isipokuwa unatendewa kazi katika mambo madogo madogo, kwa kuwa ni dalili zinazotia dhana. Tunasema kwamba zinawatia dhana nyinyi, ama Ahl-ul-Iymaan haziwatii dhana isipokuwa zinafidisha yakini maadamu zimethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi zinafidisha elimu. Hivyo haziweki dhana. Zinatendewa kazi katika mambo ya ´Aqiydah, mu´amala na mengineyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Haaiyyah, uk. 61
  • Imechapishwa: 26/08/2020