Qur-aan, Tawraat, Injiyl, Zabuur, Suhuf Ibraahiym na Muusa (´alayhimaas-Swalaatu was-Salaam) ni katika elimu ya Allaah. Vilevile vitabu vyote ambavyo Allaah ameteremsha kwa Mitume Wake, ni mamoja vile ambavyo vimetufikia na ambavyo havikutufikia, vyote hivo ni katika Maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´al). Qur-aan ni katika elimu ya Allaah (´Azza wa Jall). Elimu ya Allaah haiwezi kuwa imeumbwa. Hii ni katika hoja ambayo imewaponda Jahmiyyah. Kwa kuwa Imaam Ahmad – kama itavyokuja huko mbeleni – aliwauliza “Je, elimu ya Allaah imeumbwa?” Wakasema “Hapana”. Hivyo akasema “Basi Qur-aan ni elimu ya Allaah”. Akatumia ushahidi wa Aayah:

وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ

“Na ukifuata matamanio yao baada ya yale ambayo yaliyokujia katika elimu.“ (02:120)

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/342)
  • Imechapishwa: 26/08/2020