Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hayaa ni tawi katika imani.”

“Ukiwa huna hayaa basi fanya utakalo.”

Wale ambao wanaweka kanuni hizi – yaani kama za kina ´Ar´uur, al-Ma´ribiy, al-Halabiy n.k. – ninaapa kwa Allaah kwamba hawana hayaa. Ni juu yao kuwa na hayaa kwa Allaah, wauheshimu Uislamu, misingi ya Uislamu, manhaj ya Salaf. Waisome. Kwa sababu wengi katika wao hawajui manhaj ya Salaf. Huenda wakawa wanaisoma lakini pasi na kuifahamu na kuitendea kazi.

Ni juu ya walinganizi kumcha Allaah juu ya Ummah wa Kiislamu. Ninaapa kwa Allaah kanuni hizi hazizidishi lolote na kuitendea kazi isipokuwa upotevu na kuwa mbali na Allaah (´Azza wa Jall). Warudi katika kanuni za Kiislamu na katika dalili za Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/563)
  • Imechapishwa: 26/08/2020