Haya ndio yalisemwa na Hizbiyyuun wakati al-Albaaniy alipotoa fatwa ya Hijrah kutoka Palestina

Vilevile inahusiana na pindi Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) wakati alipotoa fatwa yake kwa watu wa Palestina. Wahuburi wote wa Jordan wakaanza kumshambulia na kumtukana na kusema kuwa ni shaytwaan.

Alikuwa ni mtu mwanachuoni, ´Allaamah, Faqiyh, Muhaddith. Anaelewa dini na mambo ya kisasa. Aliwanasihi ndugu zake wa Palestina ambao hawakuwa na maisha ua utatanishi huko. Kila siku kunakufa na kuuawa mtu. Kila siku wanakabiliana na mazito. Wakati fulani anavamiwa baba, wakati mwingine ndugu mkubwa, wakati mwingine ndugu mdogo, wakati mwingine mama, wakati mwingine msichana… Ima [sauti haiko wazi] au kuuawa. Akawaambia wamuige Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alihama kutoka Makkah ambayo ndio mji mtakatifu kabisa. Palestina iko wapi ukilinganisha na Makkah? Kwa vile hamuwezi kutekeleza dini ya Allaah, basi hameni mwende mahali mnapoweza kumuabudu Allaah. Jibu lao ilikuwa kwamba ni shaytwaan. Wakamtukana vibaya sana.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-13304
  • Imechapishwa: 26/08/2020