Ninawanasihi ndugu wasidanganyike na Khutbah za watu wa Bid´ah. Haijalishi kitu zitavuta hisia kiasi gani na kuzungumzwa vizuri kulikoje. Usidanganyike nao. Kamwe huwezi kujiamini kwa mtu wa Bid´ah. Inatosheleza kwa kule Allaah kumdhalilisha kwa Bid´ah zake. Udhalilifu huu unatosha. Vovyote Khutbah, muhadhara au kalima ya mtu  Hizbiy itavovutia na kuzungumza kwa ufaswaha, wapuuze. Himdi zote ni za Allaah kuona Allaah ametutosheleza kwa kutokuwahitajia. Haijalishi kitu hata kama analia na kuwafanya wengine wakalia kama yule Khatwiyb aliyesema:

“Haijafika wakati mbwa wa Yemen akanyamaza?”

Anamaanisha Shaykh, ´Allaamah na Muhaddith Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy (Rahimahu Allaah). Alisema hivo pindi Shaykh alikuwa bado yuhai:

“Haijafika wakati mbwa wa Yemen akanyamaza?”

Naomba kinga kwa Allaah. Anyamaze wakati wewe, ka-mtu kajinga kadogo, wazungumza? Mwanachuoni, Muhaddith na Faqiyh ambaye anautakia mema Ummah anyamaze? Kuna faida gani kwa Khatwiyb huyu ambaye huenda hata analia na kuwafanya wengine pia wakulia wakati anaposema maneno haya machafu na ya kutia kinyaa? Ndio maana ninakwambieni msidanganyike. Mnajua mtu huyu ni nani? Ni al-Muhaysiniy[1]. Usidanganyike na kisomo chake. Usiswali nyuma yake. Baadhi ya watu walikuwa wanatoka Haram ya Makkah na kufunga safari kwenda ´Aziyziyyah kuswali Tarawiyh nyuma ya al-Muhaysiniy kwenye msikiti wake.

[1] Tazama http://almohisni.com/site/

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-13304
  • Imechapishwa: 26/08/2020