Hakuna anayewatukana Maswahabah isipokuwa mnafiki tu


Swali: Ni ipi hukumu ya mtu mwenye kuwatukana Maswahabah hadharani katika vyombo vya khabari. Je, anakufuru kwa kitendo hichi au hapana?

Jibu: Msingi ni kwamba huyu hana Imani na si kwamba anakufuru tu kwa kitendo hichi. Huyu msingi ni kwamba hana imani. Hakuna mwenye kuwachukia Maswahabah mtu mwenye imani, mwenye kuwachukia na kuwatukana ni mnafiki. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuwachukia ni unafiki.”

Huyu sio muislamu. Huyu ni mnafiki hata kama atajiita kuwa ni muislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13369
  • Imechapishwa: 20/09/2020