Kumtii mke katika kumuasi Allaah

Swali: Kumtii mke katika kumuasi Muumba ni aina ya ´ibaadah?

Jibu: Ndio. Kumtii kiumbe katika kumuasi Muumba, ni aina ya ´ibaadah. Ni aina ya ´ibaadah. Hii inaitwa kuwa ni shirki katika utiifu. Lakini sio shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Lakini ni aina katika shirki. Ni juu yako kutomtii yeyote katika kumuasi Allaah, sawa mke wala mwingine yeyote. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ

“Mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.” (06:121)

Hii ni shirki katika utiifu.

Check Also

Ambaye alikuwa na zaidi ya wake wanne akifa anaswaliwa?

Swali: Mwenye kufa na yuko na wake watano au zaidi ni muislmu ambaye tuna haki …