Hajj kwa mwenye maradhi ya figo

Swali: Kuna kijana ambaye ni mgonjwa figo lake limepoza. Anaoshwa mara tatu kwa wiki na vilevile ni mtu dhaifu. Je, ni wajibu kwake kujifanyia mwenyewe hajj, awakilishe mtu mwingine amfanyie au asubiri?

Jibu: Dhahiri ni kwamba mfano wa maradhi kama haya – tunamuomba Allaah atukinge nayo sisi na nyinyi – ni kwamba hayaponi. Kwa hivyo akiwa na mali basi ni wajibu kwake kuwakilisha mtu amfanyie hajj kwa hali alitoa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1190
  • Imechapishwa: 19/07/2019