Wema waliotangulia walikuwa ni wenye kushikamana barabara na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan. Vyote viwili ni Wahy na ni wajibu kuvifuata. Hakuna yeyote katika wao alisema:

“Sunnah tu iliyoadhimishwa ndio Wahy.”

Wala hakuna yeyote alisema:

“Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayakubaliwi isipokuwa kwa dalili au hoja yenye kukubaliwa.”

Hii ni misingi mitatu:

Msingi wa kwanza: Kumtia makosani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika njia za Da´wah ambazo ni zenye kukomeka.

Msingi wa pili: Kusema kuwa Sunnah ni ile tu iliyoadhimishwa.

Msingi wa tatu: Kusema kwamba maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayakubaliwi isipokuwa kwa dalili au hoja yenye kukubaliwa.

Inatosha kumraddi maneno ya Shaykh na ´Allaamah Swaalih al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) alipoulizwa – kama ilivyo kwa sauti na kwenye tovuti yake:

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kuwa Sunnah ambayo ni Wahy ni ile iliyoadhimishwa tu na anasema vilevile kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikosea katika njia za Da´wah ambapo Mola Wake akawa amemrekebisha na kumtia adabu? Ni ipi hukumu ya maneno haya na kusoma kwa mtu huyu?

Jibu: Haya ni maneno machafu na mabaya. Haijuzu kuyasikiliza na kuyanyamazia. Huku ni kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

“Wala hazungumzi kwa matamanio yake – hayo ayasemayo si jengine isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.” 53:03-04

Huyu anamtia makosani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mambo ya dini. Mambo ya Shari´ah ni Wahy kutoka kwa Allaah. Kuhusu mambo ya kidunia Mtume anawataka ushauri Maswahabah wake. Mambo ni hivyo. Ama mambo ya Shari´ah ni kwa kukomeka (Tawqiyfiy) na ni Wahy kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

“Wala hazungumzi kwa matamanio yake – hayo ayasemayo si jengine isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.” 53:03-04

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (01/12-13)
  • Imechapishwa: 11/10/2016