Futari ya maji peke yake inazingatiwa?

Swali: Mtu akiwa amefunga Ramadhaan na anasafiri kwenda nchi nyingine na hakupata kitu isipokuwa maji peke yake. Ni vipi atatatua tatizo hili?

Jibu: Ikiwa mtu amefunga na jua likazama na asipate futari zaidi ya maji, basi akate swawm kwa maji. Kwa sababu kukata swawm kwa tende tosa au tende za kawaida ni jambo limependekezwa na sio lazima.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (5611)
  • Imechapishwa: 26/04/2020