Swali: Nimeambiwa kwamba inafaa kwa mwanamke kuswali msikitini isipokuwa kutokana na sababu inayokubalika ki-Shari´ah inayomzuia. Lakini mimi ni mtu mwenye wivu na sitaki mke wangu atoke nje na napendelea aswali nyumbani kwake. Je, nitaadhibiwa kwa wivu wangu huu na sintopewa udhuru au ni mwenye kupewa udhuru kwao?

Jibu: Haya yalimtokea ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuwa mtu mwenye wivu (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuwa hamzuilii mkewe kwa ajili ya kufanya adabu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa vovyote haitakikani kwa mtu kumzuia mkewe ikiwa hakuna kikwazo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokamana na misikiti ya Allaah.”

Afanye adabu na andiko.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 28/08/2021