Swali: Kuna Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo zinasisitiza mtu kujiepusha na fitina. Kutokana na hali ya leo ni bora kwa mtu kujiepusha na fitina au asimame juu ya haki na kupambana na wale wenye kueneza fitina?

Jibu: Ajiepusha na fitina. Lakini akitiwa katika mitihani na kukutana nayo na kuiona apambane nayo kwa elimu yenye manufaa na ubainifu. Lakini kila ambavyo mtu atajiepusha nayo ni bora na salama zaidi kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017