Kusoma kupitia mikanda na vitabu

Swali: Mtu anazingatiwa kuwa anatafuta elimu kwa kusikiliza mikanda ya wanachuoni ambao wanafafanua vitabu…

Jibu: Hapana, hapana. Huku sio kutafuta elimu. Kusoma haiwi kupitia mikanda, inakuwa kupitia wanachuoni. Mtu anatakiwa kukaa mbele yao, kuwauliza, kujadiliana nao, kuchukua elimu kutoka kwao. Elimu haichukuliwi kutoka katika mikanda na vitabu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017