Baadhi ya Aayah na du´aa anazosomewa aliyefanyiwa uchawi

Swali 05: Ni ipi dawa kwa ambaye amefanyiwa Swarf, ´Atwf au uchawi? Ni vipi muumini anaweza kukutokamana na hilo? Je, kuna du´aa au dhikr kutoka katika Qur-aan na Sunnah juu ya jambo hilo?

Jibu: Zipo aina mbalimbali za dawa:

1- Kutatazamwa kile alichofanya mchawi. Kwa mfano ikijulikana kuwa ameweka unywele mahala fulani, ameuweka kwenye kichanuo au mahala kwenginepo, basi kitu hicho kitaondoshwa, kuchomwa moto na kuharibiwa. Hivyo kitaharibika kile kilichofanywa na kitatokomea kile alichokusudia mchawi.

2- Amlazimishe mchawi kuondosha kile alichofanya. Amwambie ima aondoshe kile alichofanya au atakatwa shingo yake. Akikiondosha kitu hicho basi mtawala atamuua. Kwa sababu maoni yenye nguvu ni kwamba mchawi anatakiwa kuuliwa pasi na kumtaka kutubia. Hivo ndivo alivofanya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh). Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Adhabu ya mchawi ni kupigwa upanga.”

Vilevile wakati Hafswah, ambaye ni mama wa waumini, (Radhiya Allaahu ´anhaa) alipojua kuwa kijakazi wake amefanya uchawi akamuua.

3- Kisomo. Hakika kisomo kina athari kubwa katika kuondosha uchawi. Anasomewa yule ambaye kafanyiwa uchawi au ndani ya chombo Aayat-ul-Kursiy, Aayah zinazohusiana na uchawi zilizoko katika Suurah “al-A´raaf”, Yuunus, Twaa Haa pamoja na Suurah “al-Kaafiruun”, al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas, aombewe shifaa na afya na khaswa ikiwa ni zile du´aa zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama mfano wa:

اللهم رب الناس، أذهب البأس، واشف، أنت الشافي لا شفاء إلا شفاؤك، شفاءً لا يغادر سقماً

“Ee Allaah! Mola wa watu ondosha haya maradhi na mponye wewe ni mponeshaji hakuna shifaa isipokuwa shifaa yako, ponyo ambalo halitoacha maradhi.”

Miongoni mwa hayo ni yale ambayo Jibriyl alimsomea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo ni:

بسم الله أرقيك من كل شيء يؤذيك من شر كل نفس أو عين حاسد، الله يشفيك بسم الله أرقيك

“Naanza kukusomea kwa jina la Allaah, kutokamana na kila kitu chenye kukuudhi, na kutokamana na shari za kila nafsi au kijicho hasidi Allaah akuponye. Naanza kukusomea kwa jina la Allaah.”

Akariri matabano haya mara tatu na pia akariri kusoma:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.”[1]

al-Falaq na an-Naas mara tatu. Katika hayo pia asome yale tuliyotaja katika maji na yule aliyefanyiwa uchawi anywe kutoka humo na aoge yale yatayokuwa yamebaki mara moja au zaidi ya hivo kutokana na vile itavyopelekea haja. Kwa kufanya hivo utaondoka – kwa idhini ya Allaah. Haya yametajwa na wanachuoni (Rahimahumu Allaah). Hayo yametajwa na Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Hasan (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake “Fath-ul-Majiyd Sharh Kitaab-it-Tawhiyd” katika mlango “Yaliyokuja katika an-Nushrah”. Pia yametajwa na wengine.

4- Achukue majani saba ya mkunazi wa kijani na ayadidimize ndani ya maji na asome zile Aayah na Suurah zilizotangulia na du´aa na ayanywe na kuyaoga. Hayo yanasaidia kumtibu mume pindi anapozuiwa kutokamana na mke wake ambapo ataweka majani saba ya mkunazi wa kijani ndani ya maji na asome ndani yake yale tuliyokwishatangulia kutaja. Kisha baada ya hapo atayanywa na kuyaoga. Kufanya hivo kunasaidia kwa idhini ya Allaah (´Azza wa Jall).

Aayah zinazosomwa ndani ya maji na majani ya mkunazi wa kijani kwa nisba ya wale waliofanyiwa uchawi na aliyezuiwa na mke wake na akashindwa kumjamii ni kama ifuatavyo:

1- Kusoma al-Faatihah.

2- Kusoma Aayat-ul-Kursiy kutoka katika Suurah “al-Baqarah” ambazo ni maneno Yake (Ta´ala):

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

”Najilinda kwa Allaah, kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali. Allaah, hapana mungu wa haki mwingine isipokuwa Yeye, aliyehai daima, msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika ujuzi Wake isipokuwa kwa alitakalo. Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo – Naye ni yujuu kabisa, ametukuka kabisa.”[2]

3- Kusoma Aayah za “al-A´raaf” ambazo ni maneno Yake (Ta´ala):

قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ  وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ ۖ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ  يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانقَلَبُوا صَاغِرِينَ وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ

“Akasema: “Ikiwa umekuja na alama, basi ilete ukiwa ni katika wakweli.” Hivyo akaitupa fimbo yake na mara tahamaki ikawa joka ya waziwazi na akatoa mkono wake mara tahamaki huo ni mweupe [wenye kung´ara] kwa watazamao. Wakasema wakuu katika watu wa Fir’awn: “Hapana shaka huyu ni mchawi hodari, anataka kukuondosheni kutoka ardhini mwenu, hivyo basi mnaamrisha nini?” Wakasema: “Muakhirishe kidogo na kaka yake na tuma katika miji wenye kukusanya wakujie kila mchawi hodari.” Wakaja wachawi wa Fir’awn wakasema: “Je, tutapata ujira ikiwa sisi tutashinda?” Akasema: “Ndio, na bila shaka nanyi mtakuwa miongoni mwa wakaribu yangu.” Wakasema: “Ee Muusa! Ima utupe wewe au tuwe sisi wa kwanza kutupa?” Akasema: “Tupeni!” Basi walipotupa, waliyaroga macho ya watu na wakawatia woga na wakaja na uchawi mkuu.”  Tukamteremshia Wahy Muusa ya kwamba: “Tupa fimbo yako!” Basi mara tahamaki ikameza vyote walivyovibuni. Haki ikathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda. Basi hapo wakashindwa na wakageuka kuwa wenye kutwezeka. Na wachawi wakajiangusha wakisujdu. Wakasema: “Tumemuamini Mola wa walimwengu, Mola wa Muusa na Haaruun.”[3]

4- Kusoma Aayah za Suurah “Yuunus” ambazo ni maneno Yake (Ta´ala):

وَقَالَ فِرْعَوْنُ ائْتُونِي بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ فَلَمَّا أَلْقَوْا قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ السِّحْرُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ سَيُبْطِلُهُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ الْمُفْسِدِينَ وَيُحِقُّ اللَّـهُ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ

”Fir’awn akasema: ”Nileteeni kila mchawi hodari.” Basi walipokuja wachawi,  Muusa akawaambia: “Tupeni mnavyotaka kutupa.” Basi walipotupa, Muusa alisema: “Mliyokuja nayo ni uchawi; hakika Allaah atayabatilisha. Hakika Allaah hatengenezi matendo ya waharibifu. Na Allaah atathibitisha haki kwa maneno Yake ijapo watachukia wakalifu.”[4]

5- Kusoma Aayah za “Twaa Haa” ambazo ni maneno Yake (Ta´ala):

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَلْقَىٰ قَالَ بَلْ أَلْقُوا ۖ فَإِذَا حِبَالُهُمْ وَعِصِيُّهُمْ يُخَيَّلُ إِلَيْهِ مِن سِحْرِهِمْ أَنَّهَا تَسْعَىٰ فَأَوْجَسَ فِي نَفْسِهِ خِيفَةً مُّوسَىٰ قُلْنَا لَا تَخَفْ إِنَّكَ أَنتَ الْأَعْلَىٰ وَأَلْقِ مَا فِي يَمِينِكَ تَلْقَفْ مَا صَنَعُوا ۖ إِنَّمَا صَنَعُوا كَيْدُ سَاحِرٍ ۖ وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُ حَيْثُ أَتَىٰ

“Wakasema: “Ee Muusa! Ima utupe wewe au tuwe sisi wa kwanza kutupa.” Akasema: “Tupeni nyinyi.” Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana kwake kutokana na uchawi wao kwamba zinakwenda mbio. Basi akahisi khofu katika nafsi yake Muusa. Tukasema: “Usikhofu! Hakika wewe ndiye utayeshinda. Na tupa kile kilichoko mkononi mwako wa kuume, kitameza vile walivyoviunda. Hakika walivyoviunda ni vitimbi vya mchawi na wala mchawi hafaulu popote anapofika.”[5]

6- Kusoma Suurah “al-Kaafiruun”.

7- Kusoma Suurah “al-Ikhlaasw”, al-Falaq mara tatu na an-Naas mara tatu.

8- Kusoma baadhi ya du´aa zilizowekwa katika Shari´ah kama mfano wa:

اللهم رب الناس، أذهب البأس، واشف، أنت الشافي لا شفاء إلا شفاؤك، شفاءً لا يغادر سقماً

“Ee Allaah! Mola wa watu ondosha haya maradhi na mponye wewe ni mponeshaji hakuna shifaa isipokuwa shifaa yako, ponyo ambalo halitoacha maradhi.”

Hii nzuri. Akisoma pamoja nayo:

بسم الله أرقيك من كل شيء يؤذيك من شر كل نفس أو عين حاسد، الله يشفيك بسم الله أرقيك

“Naanza kukusomea kwa jina la Allaah, kutokamana na kila kitu chenye kukuudhi, na kutokamana na shari za kila nafsi au kijicho hasidi Allaah akuponye. Naanza kukusomea kwa jina la Allaah.”

mara tatu, ni vizuri.

Yaliyotangulia yakisomwa moja kwa moja kwa ambaye karogwa, akapuliziwa cheche za mate juu ya kichwa chake na juu ya kifua chake basi ni miongoni mwa sababu za kupona – kwa idhini ya Allaah – kama tulivyotangulia kutaja.

[1] 112:01

[2] 02:255

[3] 07: 106-122

[4] 10:79-82

[5] 20:65-69

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Akhtwaau fiyl-´Aqiydah, uk. 12-15
  • Imechapishwa: 08/08/2020