Swali: Ni ipi hukumu ya kuitwa kwa jina la Twaaha? Je, ni miongoni mwa majina yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ni jambo linahitajia dalili. Kinachodhihiri ni kwamba Twaaha ni herufi mbili miongoni mwa herufi za alfabeti na kwamba si katika majina yake. Sikumbuki dalili sahihi ya kwamba ni miongoni mwa majina yake  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 08/08/2020