Baada ya kutumia dawa ya kuzuia mimba ada yake imeparanganyika

Swali: Hedhi yangu ni siku tano au sita. Baada ya kutumia dawa ya kuzuia mimba, akaanza kuwa anajiwa na damu siku tano mpaka sita kabla ya kupata hedhi. Rangi ya damu hii inatofautiana. Kisha baadaye anajiwa na damu kwa rangi ya kawaida. Je, niache kuswali na kufunga zile siku nne tano za mwanzo au niache tu wakati wa hedhi?

Jibu: Damu hii ya kwanza ikiwa imefungamana na ya pili, inazingatiwa kuwa ni katika hedhi ambayo imezidi au kubadilika kwa sababu ya dawa unayotumia. Maadamu hakuna muda wa kutwahirika katikati ya hizo [damu] mbili, damu hiyo ya kwanza inazingatiwa kuwa ni katika hedhi. Ikiwa damu ya kwanza na ya pili zote mbili kwa pamoja hazizidi juu ya siku kumi na tano, yatakayozidi juu ya siku kumi na tano inakuwa ni damu ambayo hutakiwi kuacha swalah kwa ajili yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5428
  • Imechapishwa: 24/09/2020