Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayesema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` ataingia Peponi.”

Mwenye kusema hivo lakini haswali anakuwa ni mwenye kuingia katika mkumbo huo?

Jibu: Haitomfaa kitu. Hapa ni kwa ambaye ameisema mwishoni mwa uhai wake kisha ikachukuliwa roho yake. Huyu ndiye ataingia kwayo Peponi. Kuhusu mwenye kuisema ambapo akaacha swalah na matendo mengine, haitomfaa kitu shahaadah.

  • Mhusika: Imam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18326
  • Imechapishwa: 17/10/2021