Kusema “Aamiyn” hakukuwi katika swalah za kusoma kimyakimya

Swali: Ni ipi hukumu ya kunyanyua sauti kwa kusema “Aamiyn” katika swalah ya Dhuhr?

Jibu: Hatujui dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah wala matendo ya makhaliyfah wanne yanayojulisha juu ya kufaa kufanya hivo. Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”

Anayesema kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah basi aombwe dalili. Hakika si venginevyo kusema “Aamiyn” kwa sauti ya juu ni jambo maalum linalokuwa katika kisomo katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu kwa imamu na maamuma.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/121)
  • Imechapishwa: 17/10/2021