Ameacha mambo ya faradhi, akaibia watu kisha akatubu

Swali: Kuna mtu ameacha swalah kwa kipindi cha miaka kumi, akaacha kufunga, kutoa zakaah na akaiba. Baadaye akajutia lakini hakurudisha mali za watu na akatubu.

Jibu: Akitubu basi Allaah anamfutia yaliyotangulia. Akisilimu Allaah anamfutia yaliyopita. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ

“Waambie wale waliokufuru kwamba wakikoma watasamehewa yaliyotangulia.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kumwambia aliyesilimu:

”Umesilimu juu ya yale uliyotangulia kufanya katika kheri.”

Kuhusu mali aliyoiba anatakiwa kuwarudishia wenye nayo. Akishindwa basi Allaah atamlipia siku ya Qiyaamah. Lakini kama anaweza basi awarudishie wenye nayo. Hatolipa swawm wala swalah muda wa kuwa ametubu na akasilimu.

[1] 08:38

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21611/ حكم-من-ترك-الفراىض-وسرق-ثم-تاب
  • Imechapishwa: 30/08/2022