Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tunaona kuswali nyuma ya kila ambaye ni mwema au muovu miongoni mwa waislamu.”

Kuswali nyuma ya kila ambaye ni mwema au muovu ni miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Tofauti na Ahl-ul-Bid´ah. Tofauti na Ahl-ul-Bid´ah hawaswali nyuma ya viongozi madhalimu wala nyuma ya mtenda dhambi. Kwa sababu Khawaarij wanaonelea kuwa mtenda dhambi ni kafiri. Mu´tazilah wanaonelea kuwa ametoka katika imani na wakati huohuo hakuingia katika kufuru. Raafidhwah hawaonelei kuswali isipokuwa tu nyuma ya mtu ambaye amekingwa kukosea. Ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuswali nyuma ya watawala hata kama watakuwa ni watenda madhambi au madhalimu. Wanaswali nyuma yao Ijumaa, mkusanyiko na Idi. Hili ni khaswa pale ambapo kutakuwa hakuna imamu mwingine mbali na wao. Kwa mfano imamu wa Ijumaa katika mji ambapo hakuna isipokuwa Ijumaa moja, imamu wa Idi, imamu wa hajj katika ´Arafah pale ambapo kutakuwa hakuna imamu isipokuwa mtenda dhambi, ni sawa kuswali nyuma yake. Bali ni wajibu kuswali nyuma yake. Katika hali kama hii atakayeacha kuswali nyuma ya mtenda dhambi, basi Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuwa mtu huyu ni mzushi.

Hili ni miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah jambo ambalo Ahl-ul-Bid´ah wameenda kinyume nalo. Hii ndio sababu ya wanachuoni kuliingiza [suala hili] katika vitabu vya ´Aqiydah ijapokuwa masuala haya ya Usuwl ni katika mambo ya vitaga. Wameliingiza kwa lengo la kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/529-530)
  • Imechapishwa: 19/05/2020