16. Haijuzu kufanya urafiki na wale wanaompinga Allaah na Mtume Wake

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

La tatu: Mwenye kumtii Mtume na akampwekesha Allaah Mmoja, basi haijuzu kwake kufanya urafiki na wale wanaompinga Allaah na Mtume Wake, hata kama itakuwa ni jamaa wa karibu. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

 لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kwamba wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake – japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao. Hao Amewaandikia katika nyoyo zao imani na akawatia  nguvu kwa Roho kutoka Kwake na atawaingiza Pepo zipitazo  chini yake mito ni wenye kudumu humo. Allaah ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Zindukeni!  Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.”  (al-Mujaadalah 58 : 22)

MAELEZO

Suala la tatu miongoni mwa yale mambo ambayo ni wajibu kwetu kuyajua ni kupenda na kuchukia. Kupenda na kuchukia ni msingi mkubwa uliotajwa na maandiko mengi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ

“Enyi mlioamini! Msifanye rafiki mwandani wasiokuwa nyinyi! Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngesumbuka.” (Aal ´Imraan 03 : 118)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na wakristo marafiki – wao kwa wao ni marafiki – na yeyote atakayewafanya marafiki, basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.” (al-Maaidah 05 : 51)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wale ambao wameifanyia dini yenu mzaha na mchezo miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri – na mcheni Allaah, kama kweli nyinyi ni waumini.” (al-Maaidah 05 : 57)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu wapenzi ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya imani. Na yeyote miongoni mwenu atakayewafanya wapenzi, basi hao ndio madhalimu. Sema: “Ikiwa baba zenu, watoto wenu, ndugu zenu, wake [waume] zenu, jamaa zenu mali mliyoichuma, biashara mnayoikhofia kuharibika kwake na majumba mnayoridhika nayo ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Mtume Wake na kufanya jihaad katika njia Yake, basi ngojeeni mpaka Allaah alete Amri Yake; na Allaah haongoi watu mafasiki.” (at-Tawbah 09 : 23-24)

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ

“Kwa hakika mna kigezo chema kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye walipowaambia watu wao: “Hakika Sisi tumejitenga mbali nanyi na yale yote mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha daima mpaka mumuamini Allaah pekee.” (al-Mumtahinan 60 : 04)

Kuwapenda na kuwa na urafiki na wale wanaompinga Allaah, kunajulisha kuwa imani ya mtu juu ya kumwamini Allaah na Mtume Wake ni dhaifu. Kwa sababu sio jambo lisiloingia akilini mwanadamu akampenda mtu ambaye ni adui wa yule anayempenda.

Kufanya urafiki na makafiri kunakuwa kwa kuwanusuru na kuwasaidia juu ya ule kufuru na upotevu waliyomo. Kuhusu kuwapenda kunakuwa kwa kule kufanya matendo ambayo yana kuwapenda. Kwa ajili hiyo utamuona mtu anafanya kila aliwezalo ili apate mapenzi yao. Hapana shaka kwamba jambo hili linaiondosha imani yote kabisa au ule ukamilifu wake.

Kwa hivyo ni wajibu kwa muumini kumchukia, kumbughudhi na kujitenga mbali na wale wanaompinga Allaah na Mtume Wake ijapo itakuwa ni jamaa wa karibu. Lakini hata hivyo hili halimzuii mtu kumnasihi na kumlingania katika haki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 34-36
  • Imechapishwa: 19/05/2020