Faida ya tano: Ni jambo halikusuniwa kuyakusanya matamshi yote haya ya du´aa katika swalah moja. Mfano wa hilo ni kama zile du´aa mbalimbali za kufungulia swalah, Tashahhud na kwenginepo. Kufanya hivo ni Bid´ah. Sunnah ni mara kusoma du´aa hii na wakati mwingine kusoma du´aa nyingine. Hivo ndivyo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah ameyabainisha hayo katika utafiti wa somo la Takbiyraat katika swalah ya ´Iyd[1].

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (1/253/69).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 153
  • Imechapishwa: 07/01/2019