1 – Uvumilivu maana yake ni kuizuia nafsi wakati inapofanyiwa vibaya isiingie ndani ya mambo yaliyokatazwa.

2 – Uvumilivu umekusanya maarifa, subira, utulivu na mahakikisho. Hakuna sifa ambazo ni nzuri wakati zinapoambatanishwa kama upole na nguvu.

3 – Uvumilivu unakuwa mzuri zaidi pale ambapo mtu anakuwa mvumilivu ilihali yuko na uwezo wa kulipiza kisasi.

4 – Dhamrah amesema:

“Uvumilivu uko juu zaidi kuliko akili. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anaitwa kwao (al-Haliym).”

5 – Kama uvumilivu usingelikuwa na sifa nyingine nzuri zaidi ya kumzuia mtu kutenda madhambi basi ingelikuwa inatosha kuwa wajibu kwa yule mwenye busara kamwe kutoacha upole kwa kiasi anachoweza.

6 – Uvumilivu ni ima sifa ya kuzaliwa nayo, kujizoweza nayo au yote mawili.

7 – Mu´aawiyah bin Abiy Sufyaan amesema:

“Hakuna uvumilivu isipokuwa kwa kujipa mazoezi.”

8 – Abuud-Dardaa´ amesema:

“Hakika si venginevo elimu ni kwa kusoma na uvumilivu ni kwa kujipa mazoezi. Yule mwenye kujiwekea kheri basi huipata na yule mwenye kuigopa shari huiepuka.”

9 – Mwenye busara huwafanyia uvumilivu watu wote. Akiona hilo ni gumu basi ajifanye kuwa mvumilivu. Kwani hilo litampelekea mpaka kwenye mvumilivu.

10 – Ibn-ul-Mubaarak amesema:

“´Abdullaah bin ´Awn alitualika chakula nyumbani kwake. Wakati tulipokuwa tumekaa chini na kula akaja mjakazi wake akajitega kwenye nguo zake na sahani likamwanguka. Ibn ´Awn akamwambia: “Usiogope. Wewe uko huru.”

11 – Muhammad bin as-Sa´diy alisema kumwambia ´Urwah wakati alipotawala Yemen:

“Unapokasirika basi itazame mbingu juu yako na ardhi chini yako. Kisha mtukuze Muumbaji wavyo.”

12 – Wakati mwenye busara anapokasirika basi anatakiwa kukumbuka wingi wa uvumilivu wa Allaah kwake licha ya kukiuka kwake makatazo Yake. Hasira zake zisimfanye yeye kufanya dhambi.

13 – Ja´far bin Sulaymaan amesema:

“Alikuweko Baswrah mwanamke ambaye daima anafikwa na majanga. Tunapendezwa na subira yake. Siku moja alifikwa na msiba mzito lakini akaendelea kuwa na subira. Wakati nilipomtajia hilo akasema: “Hakuna msiba wowote unaonisibu isipokuwa hufikiri pamoja nao Moto isipokuwa unakuwa nauona kama mchanga.”

14 – Bakr bin Mudhwar amesema:

“Mtoto wa Abul-Haytham alifariki na akabaki na mtoto mchanga ambaye baadaye pia akafariki. Wakaja ndugu zake kumfariji wakati alipokuwa msikitini akasema: “Huzuni ya siku ya Qiyaamah imenifanya kutohuzunika juu ya kitu nilichopoteza wala kufurahikia kile nilichopata.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 208-215
  • Imechapishwa: 24/08/2021