42. Namna ya kusambaratisha maadui wa Mitume na wa mawalii


Lakini ukimuelekea Allaah (Ta´ala) na ukasikiliza hoja Zake na ubainisho Wake, hutokhofu na wala hutohuzunika.

إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا

“Hakika hila za shaytwaan ni dhaifu.” (04:76)

MAELEZO

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا

”Basi wapigeni marafiki wandani wa shaytwaan. Hakika hila za shaytwaan ni dhaifu.” (04:76)

Vovyote watavyokuwa na nguvu katika kuzungumza, kujadili, ustadi katika mantiki na ufaswaha lakini hata hivyo hawako katika haki tofauti na wewe ambaye uko katika haki midhali ni mwenye kushikamana barabara na Qur-aan na Sunnah na umeifahamu Qur-aan na Sunnah. Kwa hivyo tulia! Hawatokudhuru kamwe. Lakini haya yanahitajia mtu kurejea katika Qur-aan na Sunnah ndipo hatokhofu. Haijalishi kitu ni hoja kiasi gani walonazo na vitabu kwa kuwa ni udanganyifu tu. Isitoshe hoja hizi ukisoma mwanga na dalili za Qur-aan basi unaweza kuzisambaratisha vibaya sana. Hii ndio njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ

“Bali Tunaitupa haki juu ya batili inaitengua, tahamaki [batili hiyo inakuwa] ni yenye kutoweka na mtapata adhabu ya Moto kutokana na yale mnayoelezea.” (21:18)

قُلْ إِنَّ رَبِّي يَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَّامُ الْغُيُوبِ

”Sema: “Hakika Mola wangu anateremsha haki, Mjuzi wa yaliyofichikana.”” (34:48)

Haki ikivugumizwa kwenye batili inaiangamiza vovyote iwavyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 59
  • Imechapishwa: 10/12/2016