3- ´Aswr

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa katika zile Rak´ah mbili za mwanzo akisoma al-Faatihah na Suurah. Akirefusha kisomo katika ile Rak´ah ya kwanza zaidi kuliko anavyofanya katika Rak´ah ya pili[1]. Walikuwa wakionelea kuwa anafanya hivo ili watu waweze kuwahi Rak´ah[2].

Katika Rak´ah mbili za mwisho alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma kiasi cha Aayah kumi na tano, kiasi cha nusu ya yale anayoyasoma katika zile Rak´ah mbili za mwanzo katika Dhuhr. Alikuwa akifanya Rak´ah mbili za mwisho kuwa fupi kuliko zile Rak´ah mbili za mwanzo[3].

Alikuwa akisoma al-Faatihah katika zote mbili[4].

Wakati mwingine alikuwa anaweza kuwasikilizisha baadhi ya Aayah[5].

Halafu baada ya hapo anasoma Suurah tuliyoitaja katika Dhuhr.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Abu Daawuud kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh na Ibn Khuzaymah.

[3] Ahmad na Muslim.

[4] al-Bukhaariy na Muslim.

[5] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 100
  • Imechapishwa: 06/02/2017