35. Kisomo cha Qur-aan katika Maghrib

4- Maghrib

Wakati mwingine (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaweza kusoma Suurah fupi za Mufasswal[1]. Swalah zilikuwa fupi kiasi cha kwamba walikuwa wanaweza kuswali pamoja naye na kutoka na kwenda zako na bado wanaona sehemu walizosimika mikuki yao[2].

Alikuwa ametoka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) safarini akasoma Suurah “at-Tiyn” katika Rak´ah ya pili[3].

Mara nyingine (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma Suurah ndefu za Mufasswal na zile za kati na kati. Kwa mfano ilikuwa inaweza kutokea anasoma Suurah “Muhammad”[4], “at-Twuur”[5] na “al-Mursalaat”, ambazo alizisoma katika swalah yake ya mwisho aliyoswali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[6].

Wakati mwingine akisoma Suurah “al-A´raaf” katika Rak´ah zote mbili[7] na wakati mwingine “al-Anfaal” katika Rak´ah zote mbili[8].

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

[2] an-Nasaa’iy na Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[3] at-Twayaalisiy na Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[4] Ibn Khuzaymah (3/166/1), at-Twabaraaniy na al-Maqdisiy kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[5] al-Bukhaariy na Muslim.

[6] al-Bukhaariy na Muslim.

[7] al-Bukhaariy, Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/68/1), Ahmad, as-Sarraaj na al-Mukhallas.

[8] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 06/02/2017