30. Uharamu wa kuwaalika matajiri peke yake


28- Uharamu wa kualika matajiri peke yake

Haijuzu kuwaalika matajiri peke yake pasi na mafukara. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Chakula kiovu kabisa ni cha karamu ya ndoa ambacho wanaalikwa matajiri na wanazuiwa masikini. Yule ambaye hakuitikia wito basi amemuasi Allaah na Mtume Wake.”[1]

[1] Ameipokea Muslim (04/154), al-Bayhaqiy (07/262) kupitia Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inapatikana kwa al-Bukhaariy (09/201) aliyepokea kutoka kwa Swahabah. Inapata hukumu ya kupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama alivyobainisha al-Haafidhw wakati alipokuwa anaelezea maneno yake: “Wanaalikwa matajiri na wanazuiwa masikini”:

“Endapo mtu ataalika matajiri na masikini wote wawili basi chakula hichi hakitokuwa cha shari.”

Hadiyth nimeipokea katika “al-Irwaa´” na nimeitajia njia na shawahidi (1947).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 153
  • Imechapishwa: 21/03/2018