30. Mtu ashike msimamo gani juu ya kitabu “Manhaj-ul-Anbiyaa´”?

Swali 30: Mtu achukue msimamo gani juu ya kitabu kinachoitwa “Manhaj-ul-Anbiyaa´”?

Jibu: Maradhi yaliyoko ndani ya kitabu yanatakiwa kupigwa msitari. Baada ya hapo mtu ayatake maduka ya vitabu kuyasafisha na kipigwe marufuku Saudi Arabia[1].

[1] Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allaah) aliulizwa swali lifuatalo:

Swali: Mwandishi wa “Manhaj-ul-Anbiyaa´ fiyd-Da´wah ilaa Allaah” amesema:

“Nimesoma vitabu vya ´Aqiydah na kuona kuwa vyote si vyenye kuridhisha. Kwa sababu vina Hadiyth tu, maandiko na hukumu.”

Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Hili ni kosa kubwa. Vyote haviridhishi? Namuomba kinga Allaah. Vitabu vya ´Aqiydah sahihi sio vyenye kuchosha. Humo mnanukuliwa aliyosema Allaah na Mtume Wake. Ikiwa anamaanisha kuwa Qur-aan na Sunnah ni vyenye kuchosha huku ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Maneno haya ni kigonjwa na machafu.”

Swali: Ni ipi hukumu ya kuuza kitabu hiki?

Jibu: Ikiwa mna maneno haya haijuzu kukiuza. Ni wajibu kukipasua ikiwa maneno hayo yamo humo.” (Muhadhara “Aafaat-ul-Lisaan”, 1413-12-29, uliofanywa Twaaif)

at-Twuraabiy alitamka maneno kama ya Muhammad Suruur aliposema:

“´Aqiydah ya leo inatakiwa kujitosheleza kutokana na elimu ya zamani na kuielekea elimu mpya ambayo haikuwepo wakati wa Salaf.” (Tajdiyd-ul-Fikr al-Islaamiy, uk. 25)

Amesema tena:

“Ni lazima kwetu kutazama misingi ya Kiislamu. Ninavyoonelea misingi salama ya Kiislamu inaanza kwa Qur-aan ambayo inavyoonekana inahitaji tafsiri mpya. Tukisoma tafsiri za Qur-aan tutaona kuwa zimefungamana na uhalisia wa wakati ule. Hivyo hatuwezi kupata tafsiri ya Qur-aan inayoendana na wakati wa sasa.” (Tajdiyd-ul-Fikr al-Islaamiy, uk. 42)

Kwa maneno haya anachotaka ni kuwepo tafsiri ya Qur-aan yenye kuendana na matamanio ya watu katika kila zama. Hajui kuwa Qur-aan inapaswa tu kufasiriwa kwa njia zifuatazo; Qur-aan kwa Qur-aan, Qur-aan kwa Sunnah, Qur-aan kwa maneno ya Maswahabah na Qur-aan kwa muqtadha ya lugha ya kiarabu. Tafsiri ya Qur-aan haitofautiana kutegemea na wakati, hali za watu wala kwa nadharia za kielimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy