22. Matunda ya elimu: ´Aqiydah sahihi

2- Miongoni mwa matunda ya elimu ni kuwa na ´Aqiydah sahihi. Atayejifunza elimu ya Kishari´ah kutoka katika vitabu vya as-Salaf as-Swaalih, basi ´Aqiydah yake itakuwa sahihi, ujuzi wake juu ya Mola Wake utakuwa mzuri na atajua hadhi ya Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Atayemtambua Allaah ipasavyo atamcha ipasavyo. Kikubwa anachoweza mwanafunzi kufikia ni kuwa na ´Aqiydah sahihi ataponyooka katika kutafuta elimu na ikawa kujifunza kwake elimu ni kupitia vitabu vya as-Salaf as-Swaalih. Haya ni miongoni mwa matunda makubwa ambayo mwanafunzi anatakiwa kuyapupia.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016