14. Nguzo ya kwanza ya swalah


Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Nguzo ya kwanza ni kusimama kwa mwenye kuweza. Dalili ni Kauli Yake (Ta ´ala):

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

”Zichungeni swalah na khaswa khaswa swalah ya katikati na simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu.”[1]

MAELEZO

Kuhusiana na kusimama kwa mwenye kuweza, Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

”… simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu.”

Pia imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anh):

”Swali kwa kusimama. Usipoweza, kwa kukaa. Usipoweza, lalia bavu.”[2]

Vilevile imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa akiswali hali ya kusimama na akisema:

”Swalini kama mlivoniona nikiswali.”[3]

Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi kuswali kwa kukaa isipokuwa katika hali ya kushindwa. Ni wajibu kwa wanaume na wanawake wote ambao wana jukumu juu ya matendo yao kuswali kwa kusimama – wakiweza kufanya hivo – katika swalah za faradhi. Hata hivyo hakuna neno kuswali kwa kukaa kwa sababu ya kushindwa kutokana na maradhi au utuuzima. Sijui kama kuna mwanachuoni yeyote ambaye ana mtazamo mwingine.

[1] 02:238

[2] al-Bukhaariy (1117).

[3] al-Bukhaariy (631).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 98
  • Imechapishwa: 01/07/2018