Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Nguzo ya pili ni kuleta Takbiyr ya kufungulia swalah.

MAELEZO

Takbiyr ya kufungulia swalah ni kusema:

الله أكبر

”Allaah ni mkubwa.”

Swalah si sahihi iwapo hakuifungua swalah yake kwa Takbiyr. Iwapo atasimama kwa ajili ya nia ya kuswali na kuifungua swalah yake kwa Takbiyr, basi swalah haisihi mpaka alete Takbiyr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia mtu yule aliyekuwa anaswali kimakosa:

”Unaposimama kwa ajili ya swalah, eneza vizuri wudhuu´ wako. Kisha elekea Qiblah na ulete Takbiyr.”

Hivi ndivo ilivyokuja katika al-Bukhaariy na Muslim kuhusiana na mtu yule aliyekuwa akiswali kimakosa. Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ufunguo wa swalah ni twahara. Maharamisho yake ni Takbiyr na mahalalisho yake ni Tasliym.”[1]

Hadiyth ni nzuri na imepokelewa na Ahmad na watunzi wa vitabu vya Sunan kwa cheniya wapokezi ilio nzuri kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).

Kwa sababu pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akianza swalah yake kwa Takbiyr na akisema:

الله أكبر

”Allaah ni mkubwa.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:

”Swalini kama mlivoniona nikiswali.”[2]

Ni lazima kuanza kwa Takbiyr katika swalah zote. Mtu hawezi kuingia ndani ya swalah kwa njia nyingine isipokuwa kwa Takbiyr aseme:

الله أكبر

”Allaah ni mkubwa.”

Maana yake ni kwamba Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) ni mtukufu na ni mkubwa kuliko kila kitu.

[1] Abu Daawuud (618), at-Tirmidhiy (3), Ibn Maajah (275), ash-Shaafi´iy (1/34), Ibn Abiy Shaybah (1/208) na Ahmad (1006). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (55).

[2] al-Bukhaariy (631).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 01/07/2018