Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayh iwa sallam) amesema:

“Kila Mtume ana du´aa yenye kuitikiwa na wote wakaharakisha du´aa zao. Mimi nimeiweka du´aa yangu kwa ajili ya kuwaombea Ummah wangu siku ya Qiyaamah. Ataipata – Allaah akitaka – katika Ummah wangu yule mwenye kufa hali ya kutomshirikisha Allaah na chochote.”

Ameipokea Muslim.

Kuna Hadiyth nyingi mfano wa hizo. Mara nyingi Muslim amezitaja zote katika mlango mmoja katika “as-Swahiyh” yake. Pindi Sa´iyd bin al-Musayyab alipozisikia Hadiyth hizi alisema:

“Hapa ilikuwa kabla ya kuteremshwa mambo ya faradhi, maamrisho na makatazo.”

Maoni ya Sa´iyd bin al-Musayyab (Rahimahu Allaah) si hoja yoyote. Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa ni kosa kwa kuwa mmoja katika Maswahabah waliozipokea ni Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alichelewa kuingia katika Uislamu. Kwa maafikiano ni kwamba aliingia katika Uislamu mwaka ule ule Khaybar ilipochukuliwa, yaani mwaka wa 7. Wakati huo huku za Uislamu kama swawm, swawm na zakaah zilikuwa zimeshathibitishwa. Hapa ndipo mtu atajua udhaifu wa maoni yake na Allaah ndiye anajua zaidi.

Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa Hadiyth iko kwa jumla na kwamba inahitajia kufasiriwa na kwamba maana yake ni yule mwenye kusema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na akahakikisha haki na mambo yake ya faradhi. Hivi ndivyo alivyosema al-Hasan al-Baswriy.

Wengine wamesema kuwa inahusiana na yule mwenye kusema hivo wakati wa majuto na kutubia na akafa katika hali hiyo. Hivo ndivyo alivyosema al-Bukhaariy.

Hata hivyo maana yake imeshatangulia katika milango ya mwanzoni. Inatakiwa kufasiriwa kidhahiri na kwamba madhehebu ya Salaf na wanachuoni waliokuja baadaye na madhehebu ya Ahl-ul-Hadiyth ni kuwa yule mwenye kufa hali ya kuwa anampwekesha Allaah ataingia Peponi hata kama atakuwa ni mtenda dhambi na kwamba Allaah ana khiyari na mtu huyu ni kipi cha kumfanya.

Abu Ja´far amesema:

“Pindi Abu Zu´ah alipokuwa anataka kukata roho na wakati huo alikuwa amezungukwa na Abu Haashim, Muhammad bin Muslim, al-Mundhir bin Shaadhaan na wanachuoni wengine. Waliogopa kumwambie atamke shahaadah. Ndipo wakaambiana wao kwa wao badala yake kukumbushana Hadiyth. Muhammad bin Muslim akasema: “adh-Dhwahhaak bin ´Abdil-Hamiyd bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwa Swaalih.” Akasimama hapo. Abu Haashim akasema: “Bandar ametuhadithia, kutoak kwa Abu ´Aaswim, kutoka kwa ´Abdul-Hamiud bin Ja´far, kutoka kwa Swaalih.” Akasimama hapo. Wengine wote walikuwa wamenyamaza. Ndipo Abu Zur´ah akasema: “Bandar ametuhadithia, kutoka kwa Abu ´Aaswim, kutoka kwa ´Abdil-Hamiyd bin Ja´far, kutoka kwa Abu Ghariyb, kutoka kwa Kathiyr bin Qurrah al-Hadhwramiy, kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Yule ambaye maneno yake ya mwisho itakuwa ni “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” ataingia Peponi. Wakati huo huo akafa. Allaah amrehemu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 238-239
  • Imechapishwa: 28/12/2016