11. al-Albaaniy na bidii juu ya nchi ya Kiislamu

Imesemekana kwamba (Rahimahu Allaah) amesema:

“Waislamu wanatakiwa waanze mchakato wa kusimamisha nchi ya Kiislamu katika ardhi ya Allaah pana.”

Kama kweli alisema hivo, basi anamaanisha katika ardhi ya Allaah pana ambapo hakusimamishwi wala hakuhukumiwi kwa Shari´ah ya Allaah wala haidhihiri. Ni nchi ngapi ziko kwa sampuli kama hiyo! Pamoja na hivyo mimi nasema kwamba ulinganizi unaanza kwanza kwa Tawhiyd. Hayo Allaah amemwamrisha kila Mtume pale aliposema:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika Tulituma katika kila Ummah Mtume kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.” (16:36)

Kila Mtume aliyetumilizwa na Allaah kwa watu wa ulimwenguni aliamrishwa kwanza aanze kulingania katika Tawhiyd. Vivyo hivyo inatakiwa kwa kila mlinganizi aanze kulingania katika Tawhiyd kabla ya kila kitu na ahukumu kwa Shari´ah. Kama atakuwa na kundi la watu na wakaweza kusimamisha nchi ya Kiislamu – kama hawana – basi wafanye hivo. Wasipoweza kufanya hivo basi wanatakiwa kuendelea kulingania na kusubiri mpaka pale Allaah atapohukumu kati ya wao na maadui wao. Kama tayari wako katika nchi ya Kiislamu inayosaidia kulingania kwa Allaah, basi wamshukuru Allaah, waendelee kuboresha na kushirikiana na mamlaka. Wakiwa katika nchi ya Kiislamu isiyoshirikiana na walinganizi wala kuinusuru Da´wah, basi ni wajibu kwao kuendelea kulingania na kusubiri juu ya matokeo.

Kwa vovyote maneno yake ya wazi yanaweza kufahamika kimakosa kwamba Da´wah inatakiwa kuanza kwa kusimamisha nchi ya Kiislamu. Hii ni njia ya Hizbiyyuun ambao hawaelewi ulinganizi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Hatuonelei kuwa Shaykh (Rahimahu Allaah) amekusudia hivo. Pia inawezekana maneno yake yamehaririwa.

Mwishoni ni kwamba hakuna katika maneno ya Shaykh kitu kinachofahamisha kwamba anaitakia nchi hii shari. Lau kweli Shaykh al-Albaaniy angelikuwa na bidii za kisiasa na mielekeo ya kisiasa, basi hayo yangelionekana katika nchi aliyokuwa akiishi.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 17/11/2018